Mtanzania amtwanga Muingereza kwa TKO

0
66

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

BONDIA wa ngumi za kulipwa Mtanzania, Fadhili Majiha  ameshinda pambano lake nchini Uingereza kwa kumchapa TKO ya raundi ya nne Muingereza, Harvey Horn.

Pambano hilo lisilokuwa la ubingwa la  raundi nane flyweight, limepigwa usiku wa kuamkia leo ukumbi wa York  Berthana Garden  Jiji la London, Uingereza.

Ushindi huo wa Majiha unaendeleza ubabe wa mabondia Watanzania kuwachapa Waingereza  miaka ya hivi karibuni baada ya Hassan Mwakinyo kumtwanga kwa KO Muingereza, Sam Egginton, miaka mitatu iliyopita.

Source: mtanzania.co.tz