Taliban yakataza wanawake maigizo ya runinga

0
96

KABUL, Afghanistan

HUKU jumuhiya za kimataifa zikiendelea kulaani unyanyasaji wa kijinsia unaoendelea Afghanistan, Serikali ya Taliban ni kama imeziba masikio baada ya kuweka sheria mpya inayowazuia wanawake kuonekana kwenye maigizo ya runinga.

Hatua hiyo imeambatana na ile ya kuwataka wanawake walio kwenye taaluma ya uandishi wa habari, wakiwamo watangazaji, kuvaa ‘hijab’ wawapo kwenye majukumu yao.

Taliban waliokuwa madarakani mwaka 1990, walirejesha mamlaka yao Agosti, mwaka huu, baada ya vikosi vya kijeshi vya Marekani na washirika wake kuondoka Afghanistan.

Katika mwongozo mpya wa Serikali ya Kundi hilo la Kiislam, zimepigwa marufuku filamu zinazoonekana kukosoa sheria kandamizi, sambamba na zile zinazoonesha sehemu za ndani za mwili wa mwanaume.

Source: mtanzania.co.tz